Wanasema, desperate times calls for desperate measures!
Lakini wadada wa kibongo sikuhizi buana nawapenda kwa kupitiliza sana, sio kwa  kujiamini huku! 
Kuna rafiki yangu ametoka kuni surprise jana, kaniambia  kuwa alikuwa na bwana wake, kwa miaka 3 sasa, hakuona kabisa dalili ya jamaa  kumuoa.
Siku moja akaamua kumtoa out bwana wake, wakiwa wanakula, wanafurahi,  wanapata misosi ya nguvu, wakati wa dessert, rafkiangu akamwambia bwana, unaonaje tukioana?
Jamaa yake: akatoa macho, anamwuliza kweli?
Rafkiangu: Ndiao, kwanini tusioane? hatuna cha kupoteza u know na tumefahamiana vya  kutosha 
Jamaa: sawa, hamna shida! 
shogangu akafurahi hakuamini, wakaamua kwenda kumaliza show chumbani kwao, hakukuwa na  pete ya kuvishwa wala nini, na harusi yao ni Jumamosi ijayo.
Mnaona wasichana! hii ndio njia mpya ilioboreshwa zaidi ya kukufanya uolewe haraka!
Ukisuburi fairy tale utasanda!
 Romeo and Julieth Bado hawajaamka  usingizini ivooo? Usije subiri miaka 2000 kurudi kwa Yesu.
Desperate times calls for desperate measures!
Ndo ivo akina dada mjitoe ufahamu sio kunata.

			
0 comments