mtaniua jamaa, me naandika kitabu SASA HIVI, naombeni kidooogo mniache kidogo basi ni concentrate na kitabu na stori, duh!
Hii ni kwa wanaume woooote Tz, maana malalamiko kibao yapo kwenu sa sijui kuna shida gan
Wamekuja madogo 3 kila mtu analalamika Dada Penny tunabakwa tunabakwa!
Money Penny: woooow! Slow down your horses kwanza shida nini?!
Dogo wa 1: da penny wanaume wa skuhizi sijui vepee, me si unajua nipo na mpenz wangu, basi
akatokea kijana m1 akaniomba
namba nikampa, kutoa namba sio
dhambi, basi katika kuwasiliana
anaanza kuniita mpenz, mara mke
wangu, mara nataka kukuoa jaman
kutoa namba tu nishakuwa mke?!
Hajataka kujua kama nina mtu au
nini, yeye moja kwa moja
keshanifanya mkewe sasa kama sio
kubakana kisaikolojia ni nini afu
yupo serious balaa, nikamwambia
nina mtu haelewii, kumblock
imekuwa shida anapiga masimu
namba za ttcl namba za private,
namba ngeni mpaka boy wangu
keshajua namzunguka ugomvi
balaa
Dogo wa 2: me kesi yangu kama ya
dogo 1 ila me wangu kaenda extra
mile, siku 1 nimekaa na boy wangu
Mcity akatokea, baby, jaman upo
hapa waoooo akani hug, na
kunichumu kqenye mashavu
nikajinyofoa, boy wangu
anashangaa we vepee huyu nani,
huo moto wake mpaka kuja
kuuzima gadame, nilishajaza watu
kibao na security juu wanaamua
ngumi
Dogo wa 3: me hata siongei, kesi
yangu kama no 1 & 2 ila mie
niko mbele yao, uchumba
umevunjika janaaa kisa huyo
msheni kanifuatilia nikamkazia
namba sijampa wala nini, ka mind
akanizoom locations zotee akajua
home basi kila weekens yupo hapo
kama mlinzi wa nyumba
anaondoka saa 3 usiku,
mchumbaangu kuja buana
anamkuta, akaambiwa na mlinzi
huyu ana mwezi sasa anakuja kuja
hapa, ikawa ugomvi, wazazi
wameshindwa kuamua kesi maana
hata wao hawaelewi
Ivi nyie wanaume mmekuwaje?! Si mmesema wanawake tupo wengi sa ndo nini kuwabaka wadogo zetu kisaikolojia?!
Mnaingia kwenye maisha ya watu
bila hodi kwani tumekuwa choo cha
public?!
Vijana wa sikuhizi sijui
wamekuwaje hawataki kabisa
kukaa na baba zao/uncle zao/ kaka
zao wakubwa wawafundishe jinsi
ya ku approach wanawake, ndio
maana wanawake wengi wanataka
mibaba mijitu mizima maana vijana
kutongoza kwanza shida alafu
wabishi na ujuaji mwingi, uuuuwi
bora akina sie tuliolewaga enzi za
akina zaman, tumekula raha mpaka
basi sikuhizi ni mateso bila chuki
Hizi simu na technology basi wanaume wanaona wamerahisishiiiwa wanaleta mambo za ubwete, mshindweee kwa jina la Yesu, shindwa!
Mungu anawaona ivoo muache ubwetee!
Nasubiri excuses zenu sa!
0 comments