Toxic Bachelor kwa jina lingine wanajulikana kama bachelor Sugu ni zaidi ya YAHAYA, MATAPELI WA MAPENZI, ERIC MONDI wa Bongo Movie
Wanaanzia miaka 41-47, wengi wanakuwa wameamua kuwa single, hawataki kuoa, hawataki majukumu, wanapenda kupiga mechi bila kugharamia, wanatoa ahadi feki ulainike na maneno yao, ukidhani ni mkweli!
Kwa wanawake walio singo, wale singo maza, desperate ndio wamelizwa mtaani kuliko maelezo!
Rafkiangu alikutana na bachela m1, kwenye mataa ya trafiki kutoka posta wakiwa kwenye foleni, wakasalimiana wakavuka mataa wakafika ya redcross wakasimama tena
Bachela sugu akamwomba sana namba yake ya simu, rafkiangu akaamua kumpa, mawasiliano ya hapa na pale yakaanza
Baada ya siku 2 wakaanza kudeti, akampa jina la mtu ambae ni mkubwa mkubwa serikalini, rafiki yangu akalichukua lile jina akaenda kulifanyia kazi, yule bwana pia alikuwa na mambo za tuta, tuta tuta!
Tutaenda ... tutafanya... tutaishi.. tutapata na majigambo mengi ya mimi sitaki kukulala na kukimbia.. nataka fyucha na wewe ... nakupenda kikweliii .. hilo povu alilolitoa wewe mwanamke kama upo desperate lazima utaingia line na ahadi zake si unajua sisi wanawake tunapenda kusikia neno "tuta" tunadhani mwanaume akiongea hivyo unakuwa nae safari moja kumbe mwenzio akiongea neno tuta anamaanisha yeye na dyu dyu yake kama mlikuwa hamjui wanawake wenzangu habari ndio hiyo!
Tatizo toxic bachelor hakujua kuwa rafiki yangu mwenyewe ni moto wa kuotea mbali, mwendo kasi wa nchi ya Venis sio wa Dar es salaaam
Siku wamepanga kukutana kwa ajili ya mechi, rafkiangu akawa ameshaambiwa kuwa lile jina sio la yule bwana ameliiba kutishia wanawake kuwa yeye ni mkubwa awapate kiurahisi atembee nao awaachie maradhi, alishituka sana akaamua kufanya ujanja
kabla hawajaonana akaamua kuvaa pedi aliyoipaka tomato paste akaianika juani, harufu ya tomato paste ikakauka na ile rangi nyekundu ikasambaa kama rangi ya damu ya mzee, jamaa alipokagua akakuta kweli demu yupo kwenye siku zake akamvumilia kweli siku 14 alizoambiwa,
Baada ya siku 14 rafiki yangu akamwambia unajua mimi ni bikra, sijui kabisa, sijawahi kufanya kabisa huo mchezo!
Bachela sugu akakomaa nitakufundisha bebi, hautaumia, rafiki-yangu akamjibu sawa, ila nina hizi HIV Medical Test Hapa lazima tupime, la sivyo haitawezekana!
Bachela sugu akaguna mmmh!, akaona isiwe shida, akaanza kuongea oh sijajiandaa kupima, mara aseme embu ngoja kwanza akapokea simu kwa muda mrefu, baada ya simu akaaga oh nina dharura! kumbe hamna lolote ana miukimwi yake huko anaogopa kujulikana!
Alipoondoka akawa hapatikani tena kwenye simu, zile simu simu za awali hampigi tena rafiki-yangu wala sms hatumiii... ikawa mwishoo wa bachela sugu kuwepo kwenye maisha ya rafikiyangu!
Ninao marafiki zangu wengine walishapata ukimwi wamerudi kijijini kuuguaa!
Najua hali ya maisha ni ngumu sasa nchini kwetu Tanzania na naelewa wanawake waliopo singo wanapenda kusikia neno Tuta! Sio mbaya lakini akili vichwani mwenu, maana mabachela sugu wamerudije Dar sasa hivi,
Am just sayiiiiiiing!
Mjini shule!
2 comments
Duuu..hataree
ReplyDeleteHAHA
Delete