Leo amekuja mdogo m1, analalamika sana eti anataka kufa.. kisa kapenda kakataliwaa!!
Dogo: Dada Penny, me nipo na mpenz wangu tunapendana sana, tupo kwenye mahusiano miaka 6 sasa, miaka 3 ya kwanza tulikuwa chuoni, mapenzi yakawa kwenye simu, skype, whatsapp, simu..boyfriend anasoma Bondeni mimi nasoma Uganda Makerere
Tuliporudi Bongo baada ya shule kuisha tukaendelea na mahusiano ya ana kwa ana, lakini wote tumeokoka kwahiyo yale mambo ya kudonoana sijui mechi hamnaga, mpaka ndoa, tukikutana ni stori za hapa na pale, hugs na kiss za mashavu baaaasss!
Money Penny: Tobaaaaa roho yangu mieee! huku nacheka!
Dogo: Ndio wokovu sasa tunafanyaje, Yesu ndio kaagiza hivyo, sisi ni kondoo tunatii tu
Money Penny: haleluyaaa! Sasa dogo, huyo boyfriend ni shoga, hanisi au rijali?! Unauhakika boy friend wako hapigi nje kweli maana wokovu wa wanaume bwana, anaujua huyo huyo mwanaume mwenzao Yesu!
Kwanini unamfungia miguu mtu unaempenda?!
Dogo: Mimi hayo sijafuatilia, kama anapiga nje ni yeye shida ninayo mimi,
Money Penny: shida ipi sasa wewe dogo
Dogo: tatizo mimi Bikra
Money Penny: Bikra?! Una miaka mingap?!
Dogo: miaka 33
Money Penny: Tobaaa! Yesu ma Maria na Yosefu! miaka 33 na bado umepigwa bandeji, dogo hongera sana, kwaiyo wewe kama EBITOKE tu sio!?
Dogo: ndio na yeye anajua nilishamwambia mwanzo kabisa wa mahusiano yetu, ila ndio hivyo sasa wokovu unataka tufunge miguu.
Hapa nimesubiri weee naona jamaa hanioi wala dalili hamna na umri unakwenda, sasa swali langu nakuuliza NIMPE anibikiri au NISIMPE?!
Naona kama nikimpa nitamkosa hatonioa au nikimpa atanioa akiikuta au nikimpa kwasababu amesubiri sana hataona thamani yake anaweza akapiga weee akichoka anasepa..Dada penny nafanyaje?! Embu nisaidie nimpe au nisimpe?!
Eti ndugu msomaji, msaidie dogo wetu, je AMPE AU ASIMPEE?!
2 comments
Ukweli sisi wanaume tuko matabaka tofauti tabaka moja unaweza kumpa ndio ikawa sababu ya kukuoa ,tabaka la pili ukimpa ndio umempoteza na tabaka la tatu ukimnyima anaweza kuamini kuwa wewe bado uko vizuri na ndio itakua ushawishi mkubwa kwake akuoe.
ReplyDeleteIla kwa wanaume wengi wa sasa bila kumpa atakwambia vipi unataka kuniuzia mbuzi kwenye gunia??inabidi umpe ajue kama unaweza ukamudu kazi yake ,ushauri wangu muonjeshe ili apate msimamo kamili kama abaki na wewe kwa matumaini ya ndoa au aondoke zake asikupotezee muda
hahaha, akishaondoka zake si atakuwa ameondoka na lulu ya dogo au?! na akiondoka na lulu ya dogo, dogo unadhani atakuwa kwenye wakati gani ktk maisha yake?!
ReplyDelete