Oyooooooo! kama kawa kama dawa nimerudi kivingine tena, Mamaa wa Muziki, mpenzi wa Muziki
Najua kila mmoja wetu hapa anapenda mziki, ukiacha mpira kinachofuata ni mziki, uongo kweli?!
Wangapi huwa wanaendaga Mziki, Disco na Wake zao, Waume zao au Boyfriends / Michepuko yao?
kila mwezi Mimi na Mashosti tunaendaga mziki, at least kwa mwezi mara 1 au 2 kama tuna mzuka sanaaa.... maeneo yetu ya kujidai ni Hyatt Regency Club Rouge kwa DJ John the Legend!, tukitoka hapo tunaliamsha dude kwenda High Spirit alafu Next Door alafu Samaki Samaki masaki tunamalizia na Elements Oysterbay, hakuna kulala ni kuruka ruka na kucheka, kucheeeza, kuunywaa tukichoka tunakaa kwenye viti na kuanza kuangalia watu wanavyocheza, hapo tumechooka tunabusti usingizi kwa kuwacheka watu, maana wengine hawajui hata kucheza, ila ukitaka mziki uenjoy watu wanasema ucheze ovyo ovyo ndio uta enjoy!
Lakini wengine unaona kabisa wameiba waume za watu wamekuja nao, na mwibaji mwenyewe anakuwa na mzuka kweli kweli maana anavyomdandia na kumkatikia huyo mchepuko wake utadhani wapo gesti!
Dar yetu raha sana, maisha unayaweka unavyotaka ila Dar ikikuchachia utaona rangi zote za duniani!

Hapo familia zetu (Waume kwa watoto) zipo nyumbanii,
Ah! hapana chezea kulea wewe, unaweza hisi unapasuka lakini haupasuki! kila mtu achukue zamu yake alee wanawe! Beijin ya usawa kwani vepee hapo!?
Ah! hapana chezea kulea wewe, unaweza hisi unapasuka lakini haupasuki! kila mtu achukue zamu yake alee wanawe! Beijin ya usawa kwani vepee hapo!?
Sasa cha kushangaza zaidi, ukifika Disco au Mziki unakutana na mke na mume wanayarudi majoka hakuna mfano wake, kama vijana waliopo kwenye uchumba, hawachooookiiii ilo dude linmaamshwa kuanzia saa 4 usiku au 10 asbh wanaondoka.
Zamani wakati ndio tunaanza anza kutoka toka kwenda Disco / Mziki nilikuwa nawashangaa sana, maana kiiila ukitoka lazima ukutane na couples wale wale uliowaona last time kiwanja flan sasa unajiuliza hawa hawachoki au ndio maisha yao? nilipozoea walaaa, nikawa naona kawaida tu
Siku moja mke mwenzangu akanipigia simu,
Mke mwenzangu: mami mambo, jaman nakualika na shem mje mziki, kwa mwezi mara 2 au 1, msikae tu ndani mtazeeka, maisha yenyewe haya mafupi ya uncle wetu huyu, shida kila sehemu hamna hela, mje bwana tukapunguze stress, tu-enjoy sasa kabla hatuja expire na kuwa wazee
Money Penny: Poa my, lakini mziki si wa vijana ma bachela?! (Hapo namchora tu nione atasemaji, nilikuwa najua tu ataniambia twende bendi sijui twanga pepeta, wai!) Na wenye ndoa nao wanavamia fani?! (Nauliza huku namng'ong'a ila haoni, haha )
Mke Mwenzangu: ndio, skuhizi mziki ni ndoa mpya, mambo ya kisasa, tunaenda na wakati sisi wa Mujini, unajuaaa, akaanza kuhubiri kama kawaida yake, ndoa bwana unatakiwa uitengeneze wewe mwanamke vile unapenda uishi na mwenzio, zile ndoa za kizee sikuhizi hamnaga tena mjini, tushatupa kule, na hivi uzee mwisho msata na Dar wote ma Baby ndio kabisaa, jichanganyeni. wiki hii twende bendi ya yule kaka anaitwaga nani ah nimekumbukaa, Christian Bella, akituboa tunaenda Club Rouge naskia wanapiga oldies za ukweli sana!
Money Penny: Sawa my, ngoja nimpange shem wako nitakutonya siku ya kwenda.
Siku ya kwenda nilicheeekaaa! na hivi napenda kucheka yani mbavu zilipata mtanuaji!
kwanza nimekutana na wana ndoa wenzangu niliosoma nao chuo na sekondari na high school kibao ambao sikuwaona kabla, sasa hio cheza yao unaweza ukacheka mpaka upigweee! hawajuui wameshasahau sijui ndio ubize wa maisha, wanayarudije sasa majoka ya old school, mara atake kupiga sarakasi miili yenyewe ishazeeka sasa huko kwenye sakafu mtu kainama kuinuka mpaka msaada tutani, dah raaahaa sanaa! kweli Disco Liliingiliwaaaa!
Ila Club Rouge Hyatt Regency pananogaga sana muda wote,

Nikawa najiwazia; kumbe sikuhizi muziki umekuwa ndoa mpya au mziki umeingiliwa na ndoa zote?
hata sijui!...
hata sijui!...
Sasa zile hangover sasa za mziki, ukirudi nyumbani kulala unaanza kuskia zile miziki na beats moyoni mwako na maskioni mwako, mpaka unaamka mchana wake unajikuta unaimba tu mwenyewe hangover ya mziki.
kusema ukweli hangover yangu ya mziki ilikuwa ni ya huu wimbo wa London Beat, Thinking about YOOOOOOOHUUUU!
I've been thinking about Yooohuu
uuuuuu
I've been thinking about Yooohuu
Shi paw paw!
ahahaha
Enjoy the Video!
0 comments