MTAANI LEO: OLEWA NA MTU ANAEKUPENDA ZAIDI YAKO
- June 26, 2017
- By Money Penny Tz ~ Stories
- 0 Comments
Katika interview nilizofanya mtaani kuhusiana na mapenzi na mahusiano, nikakutana na mtu mmoja akaninongoneza sikio, Money Penny ni bora kufunga ndoa na mtu anaekupenda zaidi yako
Maana yake ni hivi:
Kama wewe ni mwanamke ni bora upate mwanaume anakupenda sanaa kuliko wewe unavyompenda
Wanawake sisi tumeumbiwa kupenda ipo kwenye DNA yetu sio wanaume, ukimpata mwanaume Penny anakupenda zaidi yako ume hit a jack pot! Huyo huyo mkamatie mshikilie
Ndio michezo ya watoto wa mjini sasa hivi Money Penny, kama ulikuwa haujui habari ndo hiyo! Kama unaona mwanaume hakupendi kiviiiiile unamweka pembeni kichwani unakamata DUME ingine lazima upime kwenye mizani maana ndoa sio mchezo!
Money Penny: na je ukaolewa na mtu ambae hakupendi mkaingia ndani akakupendea mkiwa ndani Hapo utasemaje?!
Mtu mmoja: mmh! We haujui tu mami, mwisho wa siku anaishia kuchepukia kwa mpenzi wake aliempeeeeeeenda lakini hakufanikiwa kuwa nae wewe ulieolewa unafanyika kuwa tuyu/ pia wa ndoa umzalie watoto, ina maana wewe haujui kuwa ndoa nyingi sa hivi vijana wamewekana ndani basi tu kwasababu huenda mmoja ya wana ndoa hakumpenda mwenzake na kwasababu alibeba ujauzito au alilogwa?! Kuja kukumbuka shuka kumekucha hamna mapenzi ndani ndoa migogoro kila siku
Angalia ndoa za watu waliopendana au mwanamme alimpenda sana demu wake kama zinaharibika utaja nambia
Sijawahi kuelewa kwanini, niliambiwa hivyo na kwanini kupenda kumuegemee mwanaume zaidi na sio mwanamke
Nyie wenzangu Mnasemaje kuhusu hili?!
0 comments