MTAANI LEO: DOGO KAMZIMIA SHUGA MAMI

  • June 25, 2017
  • By Money Penny Tz ~ Stories
  • 0 Comments





Kuna dogo mmoja jana kanifuata
Dogo: Dada Penny naomba  msaada wako na hekima yako tafadhali

Kuna dada namfuatilia mwaka wa 2 sasa lakini napigwaaa tuuu
Kupigwaaa nina maana napigwa hela zangu afu anasepaaa sipewi kitu mapenzi hatoi kila siku kalenda, kalenda na wewe

Money Penny Tz: sasa na wewe unapigwa kalenda miaka 2 upo tuu?! We dogo vepee?! kwani huyo dada ni nani labda?!

Dogo: hawa dada zetu, akina Zari wa diamond platnumz ma design amezaliwa mwaka wa 80

Hataki kunielewa kabisa, nikafuatilia sanaaa nikagundua yupo na KIBOPA mmoja mtu mzima yule KIBOPA kama hana 45 basi anachezea 50. Anamzimiiiia wakati me najua yule kibopa ana mke na watoto, hapa nataka nikamuharibie huyu demu kwa mke wa kibopa aachane nae

Money Penny Tz: ohooo usifanye hivyo dogo, huo ni utuyu (ujinga), kwani wewe una miaka mingapi  lakini?!

Dogo: miaka 27

Money Penny Tz: sasa unataka mashuga mami wa nini labda?! 
Huoni huyo kama dadako wa kuzaliwa?!

Dogo: kwani we da penny haujui kuwa wadada wakubwa ni watamu sana?! Service na Mechi zao ukilinganisha na hawa umri wetu watasubiri miaka 1000, labda wakachukue twishen kwao. We haujiulizi kwanini Diamond Platnumz hachomoki kwa Zari?!
Me naomba nisaidie Da Penny maana na wewe ni umri huo huo nipe maujanja ya kumpata yule demu basi

Money Penny Tz: mmmh dogo hili swala lako ni gumu.... siwezi uza taaluma yangu kwako nitakuwa boyaaa


Nyie mnamsaidiaje huyu dogo labda?!


mpeni ramani maana mimi nahisi dogo atakuwa anakula bangi kama mirungi, sio kwa umafia alionao?!

You Might Also Like

0 comments

all rights reserved - Money Penny Tanzania | Designed by EDUMEK SYSTEMS