MTAANI LEO: MOONLIGHT LADY

  • June 22, 2017
  • By Money Penny Tz ~ Stories
  • 0 Comments


Usiku mmoja wa Ijumaa, nikawa nimekaa na mashostiiii, 


Happy time, friday night tunaenjoy groove night na nini tunajikumbushia miziki ya kikwetu kwetu old school amaizing 
Mara akaja kaka m1, akaja moja kwa moja kwangu, 


Kaka: hey you 


Money Penny: Hi 


Kaka: naomba nicheze na wewe, maana katika wadada wote hapa mimi nimekuona wewe tu, 


Mashosti: aaaaah embu kwenda zakoo 


Kaka wa watu haogopi wala nini, kaning'ang'ania mpaka nikaenda kudance nae 


Tukiwa tunaelekea kwenye dance floor akasema she's my moonlight lady, hata sijali mtakachosema 
Mashosti wakawa wanacheka tu 


to make a long story short, baadae nikawa najiuliza, wapo wapi tena hawa wanaume wenye ujasiri wa namna hii?! Sikuhizi mwanaume akikuta wadada wamekaa 6 hajii, hata waiter hamtumiii, kwani wanaume skuhizi wamekuwaje jamaa?! 


 Wako wapi Agressive Man sikuhizi?! Wanaume Majasiri wa kujitoa ufahamu wakifukuzia wanachokitaka?! 


Skuhizi wanakaaa tu wanasubiri wadada waje, 


Ingawa yule kaka hatukuendeleza mahusiano lakini nilimpenda bure kwa kuthubutu! Me mwanaume anaejitoaga ufahamu nampenda sana, sio madomo zege na wale nduguzetu wapole kama makamasi! ahahahaha




You Might Also Like

0 comments

all rights reserved - Money Penny Tanzania | Designed by EDUMEK SYSTEMS