MTAANI LEO: NIMEOLEWA KWASABABU MIMI MZURI...

  • August 07, 2017
  • By Money Penny Tz ~ Stories
  • 0 Comments




Jana nilikuwa maeneo flan natembea tembea nashangaa jiji na nchi ya watu

Nilipokuwa nakula kwenye mgahawa, nyuma yangu walikuwa wadada wanakula wa 5, wote wanaleta ungese wa kike kike na kujisifia maisha yao walipofika mazuri ... wote wanakazi wana hela wana waume wote wana miaka yao ni 30 mpaka 33.. maongezi yao yalikuwa hivi wakimsema mwenzie ambae hajaolewa ambae hayupo


Sisi tumeshaolewa kila mmoja ana watoto 2, na tunajua waume zetu wanatupenda sana, na tumeolewa kwasababu ya uzuri wetu bila uzuri tusingeolewa sio kama shoga etu flan anaenda 34 hajaolewa na iyo sura yake mbaya ye kabakia kudate tu

Ikanibidi nigeuke niwaangalie hao wazuri wanafananaje nikakuta ndio wazuri lakini sio kiviiiiiiiileee yani hawashtui samahan kwa kusema hivyo

Yani ukiondoa makeup na hizo nguo za ghali walizovaa, sura zao zinabakia kuwa mbaya kama ya money penny hapa 😂

Baada ya dk 10 akaja huo shoga yao ambae hajaolewa akawasalimia maskini kazuri, hakana makeup lakini kazuriii aki unajua wanawake tunashida sana
Akaja na kaka m1 wakawasalimia kale kadada kakawaambia nawakaribisha kesho nalipiwa mahari nyumbani mje saa flani na wiki ijayo naolewa. Akaondoka zake na bwana wake handsome kinyamaa 

Hao madada wakabakia wanamshangaa kapataje bwana handsome wakati sio mzuri kiviiiile yule mwanaume kaona nini?! Wanalalamika pale wa natukana huyu bwanake anaonekana anamawe balaa angalia manguo aliovaa za bei mbaya
Angalia na shogaetu alivyovaa kama housegirl aibu huku wanamcheka maskini aki sisi wanawake tunashida jaman

Unajua nilichokifanya ni kuinuka na kuwaambia wale madada kwa hasira japo nchi ya watu 

"Kinachompeleka mtu kwa mume sio uzuri wala hela wala kazi ya mshahara mkubwa ulionayo wala utajiri ulionao wala nini, nyie pamoja na mimi pamoja na house girl aliepita tunakuwa na kitu kimoja tunachofanana kinaitwa CHIU  au MAKU

CHIU ndio unaotupeleka sisi kwa wanaume, ukamfanya mwanaume awe anakuhitaji kimwili   - so grow up Bitches!"

Nikaondoka nimewaacha wananishangaa mimi na wowowo langu kubwa kama gari la maji taka 😂 maana hawakuamini mwafrica ataongea vile

Afu huu ungese upo hata kwetu Africa, nani kawadanganya watoto wakike kuwa uzuri au kuwa na pesa nyingi au utajiri ndio unafanya msichana aolewe?!

Mbona waume zenu wanawacheat nyie wazuri na wanawake wenye sura mbaya kama moneypennytz hapa mitaani huko mpaka tunajiuliza ivi huyu baba kalogwaaa au?! Ina maana ameacha nini kwa mkewe mpaka akafuata kwa huyu mchepuko?!

Kiru embu niende kwa Mangi nikapate moja moto moja baridi msinichoshe mie



You Might Also Like

0 comments

all rights reserved - Money Penny Tanzania | Designed by EDUMEK SYSTEMS